Mkurugenzi
wa taasisi ya utafiti wa mambo ya afya ya CORDS ya nchini Ufaransa
Professa Nigel Lightfoot akitoa mada kwa wadau mbalimbali wa afya kutoka
katika mashirika na taasisi mbalimbali za Afrika na Ulaya
zinazoshughulikia masuala ya afya katika warsha ya siku mbili
inayofanyika mkoani Arusha kujadili njia bora za kupambana na magonjwa
ya mlipuko kama Ebola na mengineyo katika bara la Afrika na kwingineko
duniani.
Na
Mwandishi Wetu
NCHI za kiafrika zimetakiwa kuweka nguvu ya pamoja kuhakikisha zinapata
njia bora na za kudumu za kupambana na magonjwa ya mlipuko kama Ebola na
kuachana na utegemezi wa misaada kutoka nchi wahisani.
Dokta Andrew Kitua wa taasisi ya afya ya Ngalakeri ya Morogoro aliyasema
hayo jana katika warsha ya siku mbili ya kujadili njia bora na za
kudumu za kupambana na magonjwa ya mlipuko kama Ebola inayofanyika
mkoani Arusha.
Alisema
kwakuwa bara la afrika ni miongoni mwa waathirika wa magonjwa hayo
wadau husika katika sekta ya afya kwa pamoja na serikali za nchi husika
hazina budi kuwekeza nguvu katika kutafuta suluhisho la magonjwa hayo.
Alisema ingawa tayari kuna jitihada mbalimbali zinafanyika katika
mapambano dhidi ya magonjwa hayo lakini bado kumeonekana kuna changamoto
kubwa ya kukabiliana nayo katika maeneo yanayoathirika.
“Waafrika
tunahitajika kuweka nguvu ya pamoja katika kuhakikisha tunapata njia
bora na za kudumu za kupambana na magonjwa ya mlipuko kama Ebola,”
“Warsha yetu ya siku mbili inayoshirikisha wadau kutoka mashirika na
taasisi mbalimbali za afya itajadili na kubadilishana uzoefu wa jinsi ya
kupambana na magonjwa hayo na hatimaye kupata mikakati maalumu ya
kuiwekea nguvu dhidi ya mapambano hayo,” alisema Dokta Kitua.
Kwa upande wake Professa Julias Lutwan kutoka Uganda alisema nchi zote
kwa pamoja bila kujali kama zimewahi kuathirika au la zinahitajika
kujiweka tayari kukabiliana na magonjwa hayo.
Alisema
kwa afrika ukanda wa nchi za magharibi zinaonekana kupata athari hiyo
kwa kiasi kikubwa unapolinganisha na ukanda wa mashiriki lakini bado kwa
pamoja tunahitajika kujiweka sawa kwa tahadhari katika hilo.
Kwa upande wa changamoto wanazokabiliana nazo katika tafiti wanazofanya
kwa pamoja na mapambano ya jumla ya magonjwa hayo alisema mawasiliano
na kada za chini katika maeneo ya vijijini ni miongoni mwa changamoto
kubwa.
Alisema
kwa kuwatumia wataalamu mbalimbali wa mawasilino wamejitahidi kwa kiasi
kikubwa kurahisisha lugha ya mawasiliano ili jamii ya chini iweze
kupata ufahamu wa jinsi ya kupambana na magonjwa husika.
Warsha hii inayoshirikisha wadau mbalimbali wa sekta ya afya kutoka
barani afrika na ulaya imeandaliwa kwa pamoja na taasisi za afya za
SACIDS na EAIDSNet na kufadhiliwa na taasisi ya afya ya CORDS ya nchini
Ufaransa.
0 comments:
Post a Comment