Naibu Waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii Eng. Ramo Matala Makani
(kushoto)
akizungumza na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Adelhelm Meru (katikati)
ofisini kwake leo tarehe 14 Desemba 2015 baada ya kufika kwa mara ya
kwanza toka kuteuliwa kwake na Mhe. Rais Dkt John Pombe Magufuli kuwa
Naibu Waziri wa Wizara hiyo.
Katika
salam zake kwa uongozi na watumishi wa Wizara hiyo amewaomba
ushirikiano wa dhati kwa kila mmoja kutekeleza majukumu yake kwa wakati
ili kuleta maendeleo katika sekta ya Maliasili na Utalii nchini.
Ameongeza kuwa yeye binafsi hawezi kuleta maajabu Wizarani hapo bila
kupewa ushirikiano katika kazi. Pichani kulia ni Naibu Katibu Mkuu
Wizara ya Maliasili na Utalii Ndugu Selestine Gesimba.
Katibu
Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Adelhelm Meru (kulia) akitoa
taarifa fupi ya muundo pamoja na shughuli mbalimbali zinazofanywa na
Wizara ya Maliasili na Utalii kwa
Mhe. Naibu Waziri wa Wizara hiyo Eng. Ramo Matala Makani muda mfupi
baada ya kuwasili katika ofisi yake mpya iliyopo Mpingo House Jijini Dar
es Salaam.
(kushoto)
akimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Adelhelm Meru
wakati akimpa taarifa fupi ya muundo wa Wizara hiyo leo tarehe 14 Desemba 2015 . (Picha na Hamza Temba wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Maliasili na Utalii)
0 comments:
Post a Comment