Meneja Bidhaa wa Benki ya Exim Tanzania,
Bw Aloyse Maro (kushoto) akikabidhi mfano wa ufunguo wa gari kwa Meneja
Mahusiano Msaidizi wa benki hiyo Bi. Naomi Sanga (katikati) ambaye
alimuwakilisha mshindi mkuu wa kampeni ya akaunti ya
malengo ya benki hiyo aliyejishindia gari aina ya Toyota IST kwenye hafla fupi ya
makabidhiani iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam. Anaeshuhudia
ni Meneja Masoko wa Benki hiyo Bw Abdulrahman Nkondo.
Benki ya Exim Tanzania imekabidhi zawadi kuu kwa mshindi wa kampeni
ya akaunti ya malengo baada ya kuendesha droo yake ya mwisho na kubwa chini ya
usimamizi wa Bodi ya taifa ya michezo ya kubahatisha (GBT) jijini Dar es Salaam
wiki iliyopita.
Bi. Naomi Sanga ambaye ni
Meneja Mahusiano Msaidizi wa benki hiyo
alikabidhiwa funguo za gari aina ya Toyota IST kwa niaba ya mshindi katika hafla fupi ya makabidhiano iliyoandaliwa
na benki hiyo na kufanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Akizungumzia
ushindi huo wa mteja wao huyo Bi. Sanga alielezea furaha yake na kusema kuwa mpango
wa Benki ya Exim wa kuwazawadia wateja wake unaonyesha shukrani za benki hiyo
katika kutambua uaminifu na mchango wa wateja wao.
"Mshindi wetu ameupokea ushindi
huu kwa furaha kubwa japo kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wake
alishindwa kujumuika nasi leo. Ubora wa bidhaa za Benki ya Exim, huduma bora kwa wateja na viwango vinavyovutia vya riba vinavyotolewa katika akaunti hii
ya malengo vinathibitisha dhamira
ya benki hii katika kukidhi mahitaji ya
wateja wao,” alisema.
Akizungumza
wakati wa hafla hiyo, Meneja bidhaa wa Benki ya Exim, Aloyse Maro, aliwapongeza
washindi waliojizolea zawadi mbalimbali katika kipindi chote cha kampeni hiyo
huku akiwashukuru wateja waliojitokeza kushiriki katika droo hiyo.Kwa mujibu wa Bw. Maro, sambamba na zawadi
hizo kampeni hiyo iliambatana na utoaji wa riba nzuri zaidi kwa wateja
wanaofungua akaunti hiyo ya malengo.Alisema lengo la benki yake ilikuwa kuhamasisha utamaduni
wa kujiwekea akiba miongoni mwa Watanzania.
0 comments:
Post a Comment