Mgeni
rasmi Mkurugenzi wa TAMWA, Bi. Edda Sanga(kushoto) pamoja na
Mkurugenzi washirika lisilo la kiserikali nchini la International
Association of Women in Radio and Television (IAWRT) Tanzania Bi. Rose
Haji Mwalimu wakizindua ripoti ya utafiti kuhusu mwanamke au mtoto wa
kike anavyopewa nafasi hasa kwenye vyombo vya habari.
Bi
Razia Mwawanga kutoka IAWRT akifungua mkutano wakati wa uzinduzi wa
ripoti ya utafiti kuhusu wanawake wanavyopewa nafasi hasa katika vyombo
vya habari hasa hapa nchini.(Picha na Geofrey Adroph wa Pamoja blog)
Mkurugenzi
wa Shirika lisilo la kiserikali nchini la International Association of
Women in Radio and Television (IAWRT) Tanzania Bi. Rose Haji Mwalimu
akizungumza jambo wakati wa uzinduzi wa ripoti ya utafiti kuhusu
wanawake wanavyopewa nafasi hasa katika vyombo vya habari hasa hapa
nchini
Mgeni
rasmi Mkurugenzi wa TAMWA, Bi. Edda Sanga(kushoto) akiwahamasisha
wanawake kuwa na uthubutu ili kuyafikia malengo waliyojiwekea na
kutojiona hawawezi kisa wao ni watoto wa kike, kulia ni Mkurugenzi wa
IAWRT Tanzania Bi. Rose Haji Mwalimu.
Wajumbe wa IAWRT wakiangalia moja ya filamu inayohusu nafasi ya mwanamke hasa katika jamii.
Wajumbe wa mkutano huo wakiendelea kutoa maoni yao kuhusu usawa wa kijinsia katika ngazi mbalimbali za maamuzi.
Katika ripoti iliyotelewa awali na Shirika
lisilo la kiserikali nchini la International Association of Women in
Radio and Television Tanzania (IAWRT), imeonyesha kwamba wanawake au
mtoto wa kike hapewi nafasi ya moja kwa moja katika kutoa taarifa au
katika shughuli za kufanya maamuzi katika ngazi mbali mbali tofauti na
watoto wa kiume au mwanaume.
Utafiti huo umebaini kwamba mbali na
kutopewa mtoto wa kike nafasi ya kufanya maamuzi katika ngazi tofauti,
ambapo wamesema inapelekea wanaume kupata kipato kikubwa zaidi ya
wanawake.
Katika
hafla hiyo mgeni rasmi alikuwa ni Mkurugenzi wa TAMWA, Bi. Edda Sanga,
ambapo ameiomba serikali na vyombo vya habari kuwapa kipaumbele wanawake
katika ngazi tofauti tofauti za uongozi ili kuweza kuondoa lile tabaka
lililopo kati ya mwanamke na mwanaume, na pia inaweza kuchangia katika
maendeleo na mabadiliko ya nchi kiujumla.
Aliongezea
kwa kusisitizia kuwa wanawake wenyewe washirikiane na wajitume pale
wanapopata fursa katika matukio, na pale wanapofanikiwa warudi kuja
kusaidia kuinua wanawake wengine ambao bado hawajaweza kufika pale
panapohitajika.
Akizungumza Mkurugenzi wa Shirika lisilo la
kiserikali nchini la International Association of Women in Radio and
Television (IAWRT) Tanzania, Bi. Rose Haji Mwalimu alisema kwa wanawake
inabidi wajitambue na pia wajue thamani zao katika jamii ili waweze
kufikia malengo yao.
Hayo
aliyasema wakati wa uzinduzi wa Ripoti ya Utafiti kuhusu Mwanamke au
mtoto wa kike anavyopewa nafasi hasa kwenye vyombo vya habari ambapo
ilionekana mtoto wa kike hapewi nafasi sawa na mtoto wa kiume.
Hii imekuwa ni changamoto hasa kwa nchi za Afrika kutomthamini mtoto wa kike.
Pia lisisitiza kuwa licha ya juhudi nyingi
za wanahabari na taasisi za habari kuwainua wanawake na wasichana katika
vyombo vya habari mathalani Radio bado juhudi zinakabiliana na
changamoto kadhaa licha ya kuzaa matunda kwa sehemu ndogo na kupelekea
mwanaume kuwa na nafasi kubwa katika vyombo hivyo.
0 comments:
Post a Comment